Nyota wa wa muziki nchini Exray ameachia tracklist ya Album yake mpya inayokwenda kwa jina la “The Movement.”
Exray ambaye ni msanii wa kundi la Boondocks Gang ameshare tracklist hiyo yenye nyimbo 21 kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo wiki hii.
Album ya “The Movement” itakuwa ni album ya kwanza kutoka kwa Exray tangu aanze safari yake ya muziki na amewashirikisha wasanii kama Mejja,Vivian na wengine kibao.
Japo hajaweka wazi ni lini ataiachia rasmi albam yake hiyo lakini kupitia comments za watu kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kuwa na kiu ya kuipata album hiyo.