Baada ya rapa Drake kutoka Marekani kutoa taarifa ya kuwa ameahirisha kuiachia album yake ya “Certified Lover Boy” kutokana na matatizo ya kiafya.
Hatimaye rapa huyo amewapa moyo mashabiki zake kwa kupost picha akiwa studio huku watu wakiamini kwamba labda watapata wimbo mpya kabla ya albamu.
Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mashabiki wa CEO huyo wa lebo ya Ovo Sound kupata kitu kipya kutoka kwa mkali huyo wa Canada hivi karibuni au kuongezewa nyimbo nyingine kwenye albamu.