Rapa mwenye asili ya Canada Drake anazidi kuwapa moyo mashabiki zake kwa kuwaonyesha picha akiwa studio kuandaa kazi,huenda akaachia kazi mpya kabla ya kuiachia album yake ijayo kutoka studio “Certified Lover Boy”.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao waInstagram ameweka picha akiwa studio huku mashabiki zake wakiwa na imani kuwa huenda rapa huyo akaachia kazi mpya kabla ya kuachia album yake ya Certfied Lover Boy” ambayo aliahirisha kuiachia kutokana na sababu za kiafya.
Ikumbukwe mwanzoni albam hiyo ilipanga kuachiwa mwezi Januari mwaka wa 2021, lakini alishindwa kutokana na sababu alizozielezea mwenyewe ni za kiafya.
“Certified Lover Boy” inayotarajiwa kutoka mwaka huu 2021 itakuwa ni albam yake ya 6 kutoka studio.