Rapa kutoka marekani Drake ameachia rasmi EP yake mpya iitwayo “Scary Hours 2” yenye jumla ya ngoma 3.
Drake ameachia project hiyo usiku wa kuamkia jana ikijumuisha mikwaju mizito kama; Whats Next, Wants and Needs akimshirikisha Lil Baby na Lemon Pepper Freestyle ambayo amempa shavu Rick Ross.
Hizi ni dalili za ujio wa album yake mpya iitwayo “Certified Lover Boy” ambapo kama utakumbuka mwezi Januari, mwaka wa 2018 Drake aliachia project iitwayo Scary Hours yenye ngoma mbili, ikafuatiwa na album ya “Scorpion” iliyoachiwa mwezi Juni, mwaka wa 2018.