DADDY ANDREA AWATOLEA UVIVU WANAOKOSOA MUZIKI WAKE

You are currently viewing DADDY ANDREA AWATOLEA UVIVU WANAOKOSOA MUZIKI WAKE
  • Post category:Burudani

Staa wa muziki nchini Uganda Daddy Andrea amekuwa akipata ukosoaji mkubwa kutoka kwa wadau wa muziki nchini uganda tangu alipoachia video ya wimbo wake na Nina Roz iitwayo “Andele” wiki moja iliyopita .

Watu wengi wamekuwa wakihoji kwamba ubora wa video ya wimbo huo haujeafikia viwango vya kimataifa huku wakisema kwamba wimbo huo wa andele ulihitaji video bora zaidi.

Sasa akijibu kuhusu suala hilo kwenye moja ya interview Daddy Andrea amewatolea uvivu wanaodai kwamba video ya wimbo wake hauna ubora kwa kusema kwamba ni malimbukeni ambao wana fikra za kikoloni.

Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kuwataka wanaokosoa kazi zake kutofutilia nyimbo zake kwenye platforms zote za kusikiliza muziki duniani kwani ana mashabiki sugu ambao wanafurahia muziki wake.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa