DABABY AFUNGULIWA MASHTAKA YA KUMPIGA MTU HADI KUMTOA JINO.

You are currently viewing DABABY AFUNGULIWA MASHTAKA YA KUMPIGA MTU HADI KUMTOA JINO.
  • Post category:Burudani

Rapa DaBaby kutoka nchini Marekani huenda akalipishwa fidia ya takriban shillingi millioni 12.8 kwa kumpiga ngumi mmiliki wa nyumba hadi kumtoa jino.

Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba rapa huyo alikodisha nyumba kwa ajili ya kufanya video, na walikubaliana na mwenye nyumba kuingiza watu 12 tu ndani kulingana na kanuni za COVID-19.

Kinyume na masharti, DaBaby aliingiza watu takribani 40, mwenye nyumba hiyo ambaye amefahamika kwa jina la Gary Pagar alipoamua kumfuata kwa kuvunja masharti ya mkataba, mtu mmoja toka kambi ya DaBaby alimvamia na kumuangusha chini.

Baada ya hapo DaBaby alitoka kwenye gari na kumkimbiza Pagar hadi ndani ambapo alianza kwa kumuonya kutowapa taarifa polisi kisha alimtwanga ngumi ya uso hadi kumng’oa jino. Shuhuda mmoja alipiga simu kuita polisi, na DaBaby na timu yake walikimbia eneo hilo.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa