BURNA BOY ATAJWA KWENYE ORODHA YA WASANII WATAKAOTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA GRAMMY 2021

You are currently viewing BURNA BOY ATAJWA KWENYE ORODHA YA WASANII WATAKAOTUMBUIZA KWENYE TUZO ZA GRAMMY 2021
  • Post category:Burudani

Nyota wa muziki kutoka Nchini Nigeria Burna Boy ametajwa katika orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye onyesho la utoaji wa Tuzo za Grammy mwaka 2021 litakalofanyika Machi 14 mwaka huu Los Angeles, nchini Marekani

Burna Boy ni miongoni mwa wasanii wanaowania Tuzo za Grammy mwaka wa 2021 katika Kipengele ‘Best Global Music Album’.

Sanjari na hilo mwanamuziki Jhené Aiko ndiye ameteuliwa kuwa Main Host wa Sherehe hizo.

Ikumbukwe Tuzo za Grammy za 2021 awali zilipangwa kufanyika mwezi Januari mwaka huu kabla ya kuahirishwa hadi Machi kwa sababu ya ongezeko la maambukizi ya COVID-19 huko Los Angeles nchini Marekani.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa