Kaunti ya Turkana imejiunga na kaunti zingine ambazo tayari zimepitisha mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa BBI baada ya mswada huu kuwasilishwa kwenye bunge hilo mapema leo.
Akizungumza baada mswada wa BBI kupitishwa Kiongozi wa wengi katika bunge la Turkana Bethwel Lochor amesema wamefuata taratibu zote za kikatibu kupitisha mswada huo huku akipuzilia mbali madai kwamba baadhi ya viongozi na waandhishi wa habari walizuia kuhudhuria mkao wa kujadili mapendekezo ya ripoti ya bbi.
Wakati huo huo Mshirikishi wa BBI kaunti ya Turkana Beatrice Askul amewamiminia sifa madiwani kufuatia hatua ya kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mapendekezo ya ripoti ya mpango wa maridhiano (BBI).
Kauli yake imeuungwa mkono na Waziri wa Mafuta na madini John Munyes ambaye amesema hatua ya bunge ya kaunti yaTurkana kupitisha BBI kwa kauli moja imeongeza matumaini ya Wakenya kushiriki kura ya maamuzi ambayo imeratibiwa kufanyika Juni mwaka wa 2021.
Kwa upande wake Mbunge wa Loima Jeremiah Lomurukai amesema kuwa licha ya yale aliyoyataja kama propaganda na habari za kupotosha zinazosambazwa kuhusiana na mageuzi ya katiba, bunge la kaunti hiyo imesimama thabiti.