Bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi limekuwa la tano kati ya yote 47 kupitisha kwa kauli moja, mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka wa 2020.
Mswada huo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa (BBI) umewasilishwa katika bunge hilo hii leo na kupitishwa na wanachama wa bunge hilo.
Tayari Kaunti za Trans-Nzoia, Siaya, Kisumu, Homabay, na Busia zimepitisha mswada huo ambao uliwasilishwa kwenye mabunge yote 47 ya kaunti humu nchini na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ili ujadiliwe.
Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na angalau mabunge 24 ya kaunti ili uweze kuelekea kwenye hatua ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa na la Seneti.Mabunge ya Kaunti yana muda wa hadi tarehe 26 mwezi Aprili kufanya maamuzi kuhusu mswada huo wa marekebisho ya katiba.