Nyota muziki wa Injili nchini, Boss MOG ambaye pia anafahamika kama mtunzi na mwandishi wa nyimbo hapa nchini, ameweka wazi kuwa yeye ndiye mwandishi wa ngoma mpya ya Msanii Vivian akiwa na Mejja pamoja na Madtraxx iitwayo “Secret Lover”
Boss MOG ambaye alikuwa anaunda kundi la MOG, naye ana kazi yake mpya iitwayo “Amenitendea”, yenye maudhui ya kumshukuru Mungu kutokana na matatizo ambayo watu wananipitia katika maisha yao kila siku.
Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram , Boss MOG ameandika, “ Go watch this amazing song by Vivian ft the kansol written by Boss Himuselfu .”
Wimbo huo uliotoka Januari 18 mwaka huu, inazidi kufanya vizuri kwenye platforms mbali mbali za kusikilizia muziki duniani ikiwa ni kazi ya pili kutoka kwa Vivian pamoja na The Kansoul kwani kipindi cha nyuma walifanya ngoma ya pamoja iitwayo Accelerator.