Baraza la wazee Kaunti ya Pokot limetoa wito kwa Serikali kuhakikisha oparesheni ya kiusalama inayoendelea katika eneo la Kapedo inazingatia haki za kibinadamu.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo John Mwok wameelezea kusikitishwa kwao na visa vya mauaji na uhalifu katika eneo hilo huku wakionya kwamba hivi karibuni wataanda hafla ya kuwalaani vijana ambao wanawahangaisha wananchi.
Katika mazungumzo na Northrift Radio, Mwoko amekariri kwamba Serikali inapaswa kuanisha mipaka ya Kaunti za Baringo na Turkana ili kuzuia mizozo ya mara kwa mara.