Bendi ya muziki nchini Band Becca hatimae imeachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.
Band Becca ambayo inaundwa na wasanii Carol na Becky imewabariki mashabiki wake na album iitwayo “Beca Fever” yenye jumla ya ngoma 11 za moto, ikiwa na kolabo 5 pekee.
Band Becca wameshirikiana na wasanii mbali mbali wa humu nchini na nje ya nchini kama Sanaipei Tande,Mimi Mars, Femi One na Fena Gitu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Band Becca wamesema wameachia album hiyo kwa lengo la kuwahamasisha wanawake wote kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo katika jamiii.
Album ya “Beca Fever” ni album ya kwanza ya wasanii wa bendi hiyo ya tangu waanze safari yao ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music.