GAVANA NANOK AJITENGA NA HATUA YA BUNGE LA KAUNTI YA TURKANA KUPITISHA MSAADA WA PUNGUZA MZIGO

Siku chache baada ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupitisha mswaada wa punguza mzigo, Gavana wa Kaunti hiyo Josphat Nanok amepuzilia mbali shinikizo za  kubadili katiba zinazoendelezwa na kinara wa chama cha Thirdway Alliance Ekuro Aukot.

Akiwahutubia wananchi mjini Lodwar Nanok amesema maamuzi ya Bunge la Kaunti ya Turkana kupitisha mswaada wa punguza mzigo sio msimamo wa viongozi na wananchi wote wa kaunti hiyo ikizingatiwa kuwa muasisi wa mswaada huo ni mzaliwa wa kaunti ya Turkana.

Aidha Nanok amewataka wakaazi kaunti hiyo  kuunga mkono mapendekezo ya jopo lilobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga unaolenga kufanyia katiba marekebisho.

Kauli ya Nanok inakuja baada ya wakilishi wadi katika Bunge la Kaunti ya Turkana kupitisha mswaada wa punguza mzigo kwa madai kwamba utasaidia kuleta maendeleo karibu na mwananchi.

Write a Message

Your email address will not be published.

Related Posts