Mkali wa muziki nchini Arrow Boy ameingia tena katika mijadala kwenye mitandao nchini baada ya kudaiwa kuiba idea ya wimbo wa ‘Dede’ wa msanii kutoka nchini Burundi aitwaye Davis D.
Kulingana na ripoti inayosambaa mitandaoni, inadaiwa Arrow boy ametumia mdundo na ubunifu wa video wa wimbo huo kwenye wimbo wake mpya wa “Fashionista”, hivyo kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa msanii huyo amekosa ubunifu kwenye muziki wake.
Hata hivyo Arrow Boy hajetoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na watu kwenye mitandao ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii huyo aingie kwenye ugomvi na magix enga mara baada ya prodyuza huyo kudai kwamba Arrow boy hakumlipa pesa mmoja wa maprodyuza wake aliyetayarisha wimbo wa fashionista.
Ni madai ambayo Arrow Boy alizipuzilia mbali na kudai kwamba Magix Enga alitaka kutumia jina lake kujipatia umaarufu.