Msanii kutoka lebo ya WCB Rayvanny yupo tayari kuiboresha playlist yako hivi karibuni ,kwa mujibu wa Rayvanny anasema albamu yake ya kwanza kutoka studio “Sound From Africa” imekamilika kwa 99% .
Rayvanny ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika “My Albam Sound From Africa 99% ” hii ina maana muda wowote tunaweza kuipokea albam hii ya kwanza kutoka kwa msanii huyo ambaye tayari alifanikiwa kuachia EP yake inayofahanika kama #Flowers
Wakati tunakaa tayari kuipokea albam hiyo inayoweza kutoka muda wowote pia bado tuunamsubiri Rayvanny kuitambulisha lebo yake rasmi ambayo mwisho wa mwaka jana aliahidi kuja na lebo hiyo.